Karibu Usharika Wa Ubungo
Kanisa la Usharika wa Ubungo limejengwa kando ya barabara kuu ya Morogoro karibu na kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA na limepakana na jengo la RUBADA.
Usharika wa Ubungo una umri unaozidi miaka 38 hivyo na ni moja ya Sharika kongwe katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Usharika huu ulianza kama mtaa wa usharika wa Magomeni mwaka 1969 ukiwa na idadi ya Washarika takriban 10.